13 Oktoba 2020 - 13:23
El-Baradei: Mashinikizo ya kiwango cha juu zaidi ya Marekani dhidi ya Iran yamefeli

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) amekosoa vikali sera ya mashinikizo ya juu kabisa ya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusisitiza kuwa, mashinikizo hayo yamegonga mwamba.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Muhammad El-Baradei amesema hayo katika mahojiano na jarida la International na kuelekeza bayana kuwa, Marekani inapaswa kubadilisha mienendo na sera zake mkabala wa Iran.

Mkurugenzi Mkuu huyo wa zamani wa IAEA amebainisha kuwa, "mashinikizo ya juu zaidi ya Marekani dhidi ya Iran hayajafanya kazi, Washington inapaswa kujenga muamana na Iran badala ya kutumia mashinikizo."

Mwaka jana pia, El-Baradei alikosoa vikali hatua ya serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na vilevile sera za nchi hiyo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Katika mahojiano na shirika la utangazaji la BBC la Uingereza, Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa wakala wa IAEA alisema, "Wamarekani wanatumia mbinu bandia ya kuigharikisha Iran kisha wanaiangalia nchi hiyo na kuiambia njooni tufanye mazungumzo bila ya masharti yoyote." 

Taifa la Iran limeendelea kusimama kidete dhidi ya sera hizo za mabavu za Washington zinazokusudia kuwapigisha magoti wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu.

342/